Matatizo ya Waislamu nchini sio ya kikatiba

http://www.scribd.com/doc/86493055/ANNUUR1004
Matatizo ya Waislamu nchini sio ya kikatiba

– Eeh TANU yajenga nchi itaendelea kuwatesa
– Mpaka akina Kabwe, Hamad Rashid ‘wasilimu’?
– Jukwaa, Sheikh Mataka, ni kisa cha matishari (?)

Na Omar Msangi

KATIKA mambo ambayo Mzee Kitwana Selemani Kondo hatayasahau katika maisha yake,na kila akikumbuka hucheka; ni yeye kushindwa na Frank Magoba wa CUF katika kugombea ubunge, Jimb ola Kigamboni, Uchaguzi Mkuu mwaka 2000. Mzee Kitwana Kondo ni Mzaliwa wa Dar es Salaam, ni Mzaramo mzalendo. Mzee Kitwana Selemani Kondo,ni Mbunge pekee aliyeweza kuthubutu kusimama Bungeni na kuhoji juu ya mauwaji ya Mwembechai,kupigwa risasi kijana Chuki Athumani na kisha kuachwa bila matibabu huku akiwa kafungwa pingu mpaka akapooza. Ni Mzee Kitwana Selemani Kondo aliyesemea kwa uzito wake ndani ya Bunge suala la Waislamu kubaguliwa katika elimu,kutoheshimiwa muda wa swala siku ya Ijumaa na agenda nyingi za Waislamu.
Ukimuuliza Kitwana Kondo, maarufu KK,atakwambia, hayo ndiyoyaliyomponza asirudi tena Bungeni. Anajua mwenyewe nini kilitokea huko ndani ya CCM na mtandao wao wakuhakikisha kuwa miaka yote CCM inashinda kwa kishindo. Lakini swali muhimu ni kwa hawa wapiga kura wa Kigamboni. Swali ni je, wale Waislamu aliowatetea Bungeni walikuwa asilimia ngapi katika wapiga kura wa Jimbo la Kigamboni mwaka2000? Je, kwa kumnyima kura Kitwana Kondo, walitegemea kuwa Frank Magoba ndiye atatetea zaidi agenda ya OIC,Mahakama ya Kadhi, MoU,kubaguliwa Waislamu katika elimu na ajira na masuala mengine ya Waislamu? Hiyo‘Home Work’ ya kwanza Waislamu wakae nayo wakati wakichakarika na mabadiliko ya katiba.Sheikh Ilunga aliwahi kutaja kisa cha yule mbunge wa Urambo (sina hakika kwamba ni kweli au ni mzaha tu) ambaye baada yakumsikia mbunge mwenzake wa Zanzibar akisema kuwa tatizo la Bandari ya Zanzibar ni matishari, aliposimama naye akasema, Mheshimiwa Spika nami nasema hata Urambo nao wana tatizo la matishari. Mbunge mwenzake aliyekuwa pembeni akambonyeza,wewe unajua tishari ni nini? Urambo kutakuwaje na matishari? Mheshimiwa huyo, wakati ule Ndugu,uheshimiwa ulikuwa bado,akakazia hoja yake kwakujiamini na kwa kupazasauti zaidi, “hata kama siijui hiyo matishari, lakini nasema Wananchi wa Urambo naowana shida ya matishari.”Hizo zilikuwa zile zama Bunge likiwa Karimjee Hall Spika akiwa Chifu Adam Sapi Mkwawa.Sasa labda tujiulize, sisi tulipoingia katika vyama vingi, tuliingia na agenda gani? Je, tulikuwa tukivihitaji vyama? Au ni mbunge wa Urambo kutaka tishari kwa vile wa Unguja anataka?Kama si mambo ya Mbunge wa Urambo kutaka matishari,vipi Waislamu wa Kigamboni wamnyime kura KK aliyetetea agenda za Waislamu Bungeni wakampe Frank? Inaweza kujengwa hoja kuwa ilikuwa siasa za vyama kuwa ilikuwa ni suala la CCM vs CUFna ikawa CUF ndiyo yenye nguvu. Hiyo si kweli. Kama ingekuwa hoja ndiyo hiyo,huko Tunduru, Pwani na Kusini yote mpaka Tanga,CUF isingekosa wabunge.Waislamu walio CUF walimnyima kura KK kwa sababu waliingia CUF bila ya agenda zaidi ya kutaka tishari. Katika hali hiyo,wakawarahisishia kazi yao wale walioingia katika vyama na agenda ambao kwao hoja sio chama gani unaingianacho Bungeni, bali muhimu ni kusimamia agenda ya Kanisa. Na hapana shaka ndio hao hao ambao pamoja na kuipa CUF ubunge Kigamboni na Bukoba Mjini, walihakikisha kuw ahaipati Jimbo jingine Bara hata pale ambapo ilikuwa wazi kwamba ni ngome ya Ngangari.Kama tutakumbuka vizuri,tarehe 10 Februari, 2012 siku ya Ijumaa, ndiyo siku Bunge lilipokuwa linafungwa likisubiri kikao cha Aprili.Ilifika muda wa Khatibu kupanda katika Mimbar kuanza Khutba ya Ijumaa,alisimama Spika Mheshimiwa Anne Makinda na kutoa hoja.Katika maelezo yake Spika alisema kuwa, kwa kuwa siku hiyo ndiyo ilikuwa ya kufunga Bunge na kwa kuwa bado kulikuwa na mambo mengi ya kujadili, anaongeza muda wa majadili nao kwa nusu saa (dakika 30) kabla ya kwenda mapumziko.Wakati anatoa maelezo hayo ilikuwa saa 6 na dakika 50.Akiongeza dakika 30 ni kuwa Bunge litaendelea mpaka saa 7 na dakika 20. Khutba ya Ijumaa ishamalizika ni Iqama inasimama swala ya Aljumaa.Akisimulia jambo hili katika moja ya mawaidha yake, Sheikh Ilunga Hassan Kapungu anasema kuwa alichokuwa ametarajia ni kuwa wabunge vijana machachari kama Zitto Zuberi Kabwe angesimama na kutaka mwongozo waSpika. Kwamba, Mheshimiwa Spika, huu ni muda wa swala ya Al Jumaa na wewe unaongeza muda hadi saa 7 na dakika 20, nini mwongozo wako juu ya haki ya Wabunge Waislamu kwenda kuswali na Haki yao kushiriki mjadala Bungeni katika dakika hiz i30 ulizoongeza. Lakini wapi.Akakuta kumbe ujasiri wa Zitto ni kutoa tu Hoja binafsi ndeeefu juu ya mashamba ya mkonge na kuchachamaa katika kusimamia fedha za mashirika ya umma.Ilunga anasema akadhani huenda Uislamu wa wabunge wa Bara labda mwepesi, lakini Hamad Rashid na wenzake kutoka Unguja na Pemba,hawatakubali. Watasimama kuomba mwongozo wa Spika, bunge lisimame Wabunge Waislamu wakawahi Ijumaa.Wapi, wote kimyaa!Sasa labda tujiulize, wapi Katiba ya Nchi, hii iliyopo hivi sasa, inamlazimisha Mbunge Muislamu kushiriki kikao wakati Imam yupo katika Mimbar siku ya Ijumaa?Kifungu gani katika Katiba ya Nchi kinampa ruhusa, nguvu na ujasiri Spika wa Bunge Anne Makinda apuuzilie kwa mbali uhuru na haki ya wabunge Waislamu ya kwenda kuswali?Hiyo ‘Home Work’ ya pili,Waislamu turudi Diamond Jubilee, na Jukwaa letu la Katiba, tukajadili.Hivi tunavyochakarika na kutaka Katiba Mpya tukidhani (tukijidanganya)kuwa ndiyo itatupa OIC,Mahakama ya Kadhi,Mapumziko Ijumaa, kuondoa ubaguzi katika elimu na ajira; serikali inaendelea kutoa mabilioni ya shilingi kuzipa taasisi za Kikristo kupitia ile MoU. Badala ya serikali kujenga, kuboresha na kuimarisha hospitali zake za Wilaya, Mikoa na zile za rufaa, inachukua fedha za walipa kodi na kuzipa taasisi za Kikristo. Lakini zaidi ya hivyo kwa mujibu wa MoU, serikali huwajibika pia kuwatafutia Wakristo wafadhili na kuwapa nafasi za upendeleo vijana wa Kikristo katika nafasi za masomo katika vyuo vya serikali.Wapi katika Katiba hii iliyopo inatoa ruhusa kwa serikali kwamba ikisha kusanya kodi kutokakwa Waislamu na Wakristo,ikae pembeni na Wakristo pekee na kuwapa fungu la kuendesha shule na hospitali zao! Wapi Katiba hii inatoa maelekezo kwamba, serikali yetu iwe na makubaliano na Wakristo mithili ya zile“Concordats” za Vatican na Mussolin pamoja na Adolf Hitler?Hili ni swali jingine ambalo pengine tumwombe Sheikh Khamisi Mataka na Masheikh wake aliowakutanisha pale Hoteli ya Lamada na watoa mada Profesa Safari na Dr.Mvungi, watufafanulie.Hoja ni kwamba Katiba hii iliyopo ina kifungu ambacho kinasema ni Marufuku mtu yeyote kubaguliwa (aukupewa upendeleo) kwa sababu ya dini yake, rangi,kabila, na mahali anapotoka,lakini bado Waislamu wanabaguliwa huku Wakristo wakipendelewa kama ilivyo katika hii MoU. Kitu gani kinawapa Waislamu tamaa kwamba hiyo Katiba Mpya itawapa haki na kuwaondolea matatizo yao?Katika Ilani ya CCM ya mwaka 2005, CCM waliahidi kuwa wakirejea madarakani watashughulikia suala la Mahakama ya Kadhi. Swali ni je, baada ya CCM kushinda,kuna mahali popote ilitaja tena jambo hilo? Na Waislamu walipohoji CCM ilijibu nini?Hoja hapa sio Ilani inasemanini kama ambavyo hoja sio tu Katiba Mpya au Katiba ya Zamani, lakini muhimu pia ni nani anasimamia Katiba hiyo? Nani ana mamlaka yakusimamia hiyo Katiba? Naniameshikilia mpini? Nani ana mamlaka ya kusema lipi lifanyike na lipi marufuku?Katika suala la OIC, baadaya kutumia fedha nyingi za walipa kodi kuchunguza na kutafiti uzuri na ubaya wa kujiunga na taasisi hiyo ya Kiislamu ya kimataifa,serikali kupitia Waziri wake wa Mambo ya Nchi za Njena Ushirikiano wa Kimataifa,Mheshimiwa Bernard Membe alitoa taarifa akisema kuwa serikali imeona jambo hilo halina tatizo ila manufaa,hivyo (itajiunga).Kauli hiyo Mheshimiwa Membe hakuitoa barabarani,kijiweni, maskani au katika porojo katika vilabu vya ulevi(kwenye baa). Aliongelea Bungeni. Kwa hiyo ni kauli rasmi ya serikali.Nini kilifuata! Aliitwa naAskofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo na kuambiwa OIC marufukuTanzania. Sasa ukitaka kugombana na Mheshimiwa Membe, nenda kamuulize habari za OIC.Tunataka Masheikh wetu akina Mohammed Issa ambao pengine baadhi yao hivi sasa wanapigana vikumbo kutaka kuingia katika ileTume itakayoteuliwa na Mheshimiwa Rais,watuambie, wapi Katiba hii ya sasa inasema ruhusa Tanzania kuwa na Ubalozi wa Vatican lakini marufuku kujiungana Taasisi za Kimataifa za Kiislamu (kama OIC)?Kifungu gani katika Katiba hii tuliyo nayo kinasema kuwa Askofu Mkuu atakuwa ndiye mwenye kauli ya mwisho juu ya masuala mbalimbali ya serikali. Kifungu gani cha Katiba tuliyo nayo kinampa mamlaka Kadinali Pengo kutengua maamuzi yaserikali? Sheria gani na kanuni gani katika taratibu, sheria na maadili ya utumishi wa Umma, yanampa maelekezo Mtumishi wa Serikali kwamba pamoja na sheria na taratibu za kiserikali, lakini azingatie Askofu anasema nini na kwamba inapotokea msimamo wa serikali unapingana na wa Askofu, basi atupilie kwa mbali wa serikali ashike wa Askofu.Labda nisirefushe sana.Niseme kuwa hoja hapa sio Waislamu wasishiriki mchakato wa mabadiliko ya Katiba. Washiriki. Lakini ipo dhana potofu inajengeka kuwa Katiba Mpya ndiyo itaondoa matatizo ya Waislamu. Itawapa OIC,Mahakama ya Kadhi, kufuta MoU n.k. Sio kweli. Matatizo ya Waislamu katika nchi hii ni makubwa na mazito. Si ya kutatuliwa na Katiba kwa sababu hayakusababishwa na Katiba.Wale Waislamu pale Bungeni, walishindwa kuomba mwongozo wa Spika kuhusu swala ya Ijumaa kwa sababu, waliingia Bungeni bila ya Uislamu wakati Katiba iliyopo inawaambia kwamba wana uhuru wa kuabudu.Walitupa Uislamu ndio wakaingia Bungeni kinyume na matakwa ya Katiba.Spika Anne Makinda,hakuona vibaya kuwanyima Waislamu haki yao ya kwenda kuswali, kwa sababu aliingia Bungeni na Ukristo wake.Hakujali kwamba Katiba na Sheria za nchi zinazosimamia Bunge na kiti chake cha Uspika zinamkataza kuwanyima Wabunge haki yao ya kwenda kuswali Ijumaa.Hii yote ni kutokana na sababu kwamba wakati Waislamu wakiimba, Eeh TANU yajenga nchi, TANU aah, huku wakimshambulia Mzee Suleiman Takadiri kwa kumtuhumu Mwalimu Nyerere kwamba ataleta udini, Wakristo waliingiaTANU na Ukristo wao.Wakati Waislamu wakiuza kadi za TANU Misikitini,lakini wakishiriki siasa bila Uislamu, Nyerere alikuwa akipeleka salamu kwa Baba Askofu Kardinali Rugambwa kumhakikishia kwamba yeye ni Mkatoliki safi, hatalisaliti kanisa lake na kwamba atafanya kila awezalo,kuhakikisha kuwa Kanisa Katoliki linakuwa na nguvu Tanzania.Nyerere aliingia TANU na Ukatoliki wake. Nyerere aliongoza CCM na kukaa Ikulu na Ukatoliki wake.Ukisoma kitabu cha Padiri John Sivalon na kile cha Profesa Njozi, “Muslim and State in Tanzania”, jambo moja lipo wazi. Kila Mkristo aliyepo serikalini, kaingia na Ukristo wake. Lakini kubwa zaidi, Kanisa kwanza, serikali baadae. Kanisa kwanza,CCM, CHADEMA baadae.Kanisa kwanza Tanzania baadae.Sasa njoo upande wa Waislamu. Muislamu akishaingia katika siasa nahasa akipata cheo katika Chama na serikali, dini huweka pembeni. Na ukimjia na jambo la Kiislamu anaona kama unataka kumuharibia. Wakati Mawaziri wenzao, Makatibu Wakuu, Wakurugenzi na Wakuu wa Mikoa wenzao, ni Walei, Wazee wa Kanisa na Mawakala wa Kanisa ndani ya serikali; wao wapo mbali na Waislamu wenzao wakibakik uwalaumu kwamba hawana mipango.Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia amepewa Nishani na Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani,Baba Mtakatifu Benedikto wa 16. Nishani hiyo ni kwa kutambua mchango wake na utumishi wake kwa Kanisa Katoliki wakati akiwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.Sasa maadhali tutaendelea kuwa na akina Joseph serikalini na COBA wengine,huku kwa upande mwingine wanaowakilisha Waislamu serikalini ni sampuli ya akina Makamba walioitikia na kutii maelekezo ya Paroko Lwambano, ije Katiba Mpya na nzuri itakavyokuwa,dhiki na taabu ya Waislamu itakuwa pale pale.Swali laweza kuwa,tutawapataje Waislamu wakupigana vibega na akina‘Joseph’ serikalini, Bungeni na katika vyama vya siasa? Jibu jepesi na la kweli,ni kujiuliza, Wakristo waliwapataje akina Anne Makinda?Kila Muislamu hiv isasa ni mwanaharakati.Ni Mwanada’wah.Ni Mujahidina. Lakini wanaharakati sisi tungependa sana kuona ghafla tunakuwa Omar Mukhtar tukipambanana Wataliano. Tunaona fahari tukiangalia filamu ya Omar Mukhtar na kutamani kuona wanaharakati sisi tukiwa na akina Omar Mukhtar mitaani, serikalini na katika CCM na Chadema.Lakini kabla ya Omar Mukhtar kuingia katika uwanja wa mapambano na Wataliano, anaonyeshwa akiwa katika darasa za vibarazani akisomesha nakulea watoto. AkiwapaTawheed, mtizamo na kuwajenga kuwa Waislamu kwanza kabla ya kuwa Walibya.Sisi hii kazi tunaiona ngumu.Tunaona tunachelewa.Tunawasubiri akina Kabwe wakishaingia Bungeni,ndio tuwatarajie wapiganie agenda za Waislamu.Pamoja na agenda za majukwani na Diamond Jubilee, tujue kuwa Program za kila siku za kuwaendea Waislamu mitaani, vijijini na katika taasisi za elimu kuwaelimisha, kuwalea na kuwajenga wajitambue na watambue wajibu wao,ndipo ilipo nusura yetu.Kama ni kuingia Chadema,Bungeni, vijana wain
gie na Uislamu wao. Wakiwa katika biashara au katika ajira serikalini na katika taasisi binafsi, Waislamu waingine na Uislamu wao.Lakini pia tuzingatie kuwa muhimu kwetu kwa sasa hivi ni kupambana namfumo kristo. Ije Katiba yoyote itakayokuwa, maadhali msimamizi wa Katiba hiyo atakuwa mfumo kristo,hatuendi kokote. Ila tujue kwamba tatizo halipo tu kwa waheshimiwa Wabunge na Mawaziri Waislamu. Hata kwa sisi Waislamu mitaani na tunaojiita Waislamu wanaharakati. Tunapanda mabasi tupo kimyaa watu wa miziki ya Injili wakitamba katika video vilivyo katika mabasi ya kwenda Arusha,Moshi, Mwanza, Mbeya,Dodoma n.k. Mbona hatusemi zifungwe au iwekwe na Qur’an au kanda za Maalim Bassaleh na Kishki? Kukaa kwetu kimya tuna tofaut igani na wale waheshimiwa wabunge walioshindwa kumwambia Spika kuwa wakati wa swala ya Ijumaa umefika?Kwa hali hii, tutashiriki siasa za vyama vingi,tutashiriki katika mchakato wa katiba mpya; lakini mwisho wa yote tutaishia katika ule msemo wa vijana,“hata ukinawa huli.”

Advertisements

One thought on “Matatizo ya Waislamu nchini sio ya kikatiba

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s